Sera ya Faragha

Privacy & Data Protection Policy

Sera hii ya faragha inaeleza kwa uwazi jinsi M.W. MAJAMVI ("Sisi", "Jukwaa") inavyokusanya, kuhifadhi, na kulinda taarifa zako unapofikia na kutumia tovuti au huduma zetu za uchambuzi wa michezo. Tunaheshimu sana faragha yako na tunafuata sheria za ulinzi wa data za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ufafanuzi Muhimu: M.W. MAJAMVI ni jukwaa la kidijitali la takwimu za michezo na utabiri wa mpira wa miguu. Sisi si kampuni ya kubeti, hatupokei dau wala kuweka amana za kamari.

1 Taarifa Tunazokusanya (Information We Collect)

Tunakusanya taarifa pale unaposajili akaunti au kununua maudhui ya kidijitali:

  • Taarifa za Usajili: Jina la mtumiaji (Username), namba ya simu ya mkononi, na barua pepe (Email).
  • Taarifa za Malipo: Namba ya simu ya mtandao unaotumia kufanya malipo (kwa mfano Vodacom, Tigo, Airtel, Halopesa) na namba ya kumbukumbu ya muamala (Transaction Reference/Order ID).
  • Kumbuka: Hatuhifadhi PIN ya simu yako kamwe. PIN yako inaingizwa kwenye menyu ya USSD ya simu yako na inachakatwa moja kwa moja na benki/kampuni yako ya simu kupitia Selcom Gateway yenye kiwango cha kimataifa cha usalama (PCI-DSS).

2 Madhumuni ya Kutumia Taarifa Zako

Taarifa zako zinatumika kwa mambo yafuatayo pekee:

  • Kukamilisha na kuthibitisha ununuzi wa mikeka (analytical tips) kwa usahihi.
  • Kuhifadhi historia ya mikeka uliyoinunua ili uweze kuitazama wakati wowote chini ya "My Slips".
  • Kukusaidia kubadilisha au kuweka upya nenosiri (Password reset) iwapo utalisahau.
  • Kuzuia vitendo vya ulaghai, majaribio ya uvunjaji wa usalama, au akaunti bandia.

3 Ulinzi wa Data & Usalama (Data Security)

Tunatumia viwango vya juu vya usalama vya kielektroniki ikiwemo SSL 256-bit Encryption, hashing ya nenosiri (Password Hashing kutumia BCRYPT), na firewall kuzuia ufikiaji usioidhinishwa. Nenosiri lako halijawahi na haliwezi kusomwa na mtu yeyote, ikiwemo wasimamizi wa mfumo.

Hatuuzi wala kukodisha taarifa zako binafsi kwa mtu au shirika la biashara la nje chini ya mazingira yoyote.

4 Viungo vya Nje (Third-Party Links)

Tovuti yetu inaweza kuwa na nembo au viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti huru za makampuni ya kubeti yaliyosajiliwa kisheria nchini Tanzania. Hatuna mamlaka juu ya sera za faragha za makampuni hayo na tunakushauri usome sera zao unapotembelea tovuti zao.

5 Haki Zako (Your Rights)

Una haki ya kupata, kurekebisha, au kuomba akaunti yako ifutwe kwenye seva zetu wakati wowote kwa kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi kupitia ukurasa wetu wa Support.

HOME MY SLIPS PROFILE